KATIKA KOZI HII UTASOMA MODULE 4 ZIFUATAZO
MODULI NAMBA 1: MUUNDO NA MIFUMO YA TAASISI
MODULI NAMBA 2: RASILIMALI ZA TAASISI
MODOULI NAMBA 3: MIRADI YA TAASISI
MODOULI NAMBA 4: TEHAMA(TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO
MUONGOZO KUHUSU ELIMU KWA NJIA YA MASAFA
WALENGWA WA KOZI HII NI:
Ni Masheikh na viongozi wote kuanzia Mkoa, Wilaya, Kata, Misikiti, JUVIKIBA, Umoja wa Wakina mama Bakwata , walimu wa madarasa, maimamu na wale wote watakaohitaji maarifa kuhusu uongozi, utawala bora na Tehama na kupata cheti rasmi kinachotambuliwa na taasisi za kiislam Tanzania kilichosaininiwa na MUFTI wa Tanzania.
USOMAJI, UPIMAJI ,KUTUNUKU NA MADARAJA YA KUTUNUKU
USOMAJI
Kiongozi atasoma moduli hizi tatu kwa njia ya masafa (mtandaoni) kupitia tovuti ya chuo cha BAKWATA MTANDAONI kwa kupakua (download) kitabu cha moduli kisha atasoma moduli moja moja na kujibu maswali ya moduli husika. Pia, kupitia video ambazo zitawekwa kwenye tovuti.
UPIMAJI
Kiongozi baada ya kusoma moduli, atapimwa ufahamu wake kwa kujibu maswali baada ya moduli. Kila moduli itapimwa kwa uzito wa alama 100, hivyo ufaulu wa kiongozi utapimwa kupata alama 50 kuwa amefaulu moduli husika. Alama chini ya 50 maanake moduli hiyo hajafaulu. Kiongozi akimaliza kujibu maswali atatakiwa kuyatuma kwa njia ya mtandao (email) ili yapate kusahihishwa.
KUTUNUKU
Baada ya kukamilisha mafunzo ya uongozi na utawala bora, kiongozi atakayefaulu moduli zote tatu atatunukiwa cheti cha kufaulu kwake. Wastani wa ufaulu kwa moduli zote tatu ni alama 50. Maanake kama mduli zote tatu zikijumlishwa kwa pamoja kasha kugawanywa kwa tatu, wastani ukifikia 50 kiongozi atakuwa amefaulu na kuwa na sifa ya kutunukiwa.
Mfano kama moduli ya kwanza amefaulu kwa alama 70, moduli ya pili kwa alama 60 , moduli ya tatu kwa alama 80 na moduli ya 4 kwa alama 75, hivyo wastani wa jumla wa kutunukiwa ni 70 ( maanake 70 + 80 + 60 + 75= 285. Hizo alama 285 gawia kwa 4 ni sawa na alama 71.25). Hii ni kuweza kumjengea ufaulu kiongozi kwa sababu kuna moduli ambazo anaweza kuwa amezifahamu zikambeba kufaulu kwa zile moduli ambazo atakuwa hajazifaulu vyema.
Cheti kitatolewa na kusainiwa na Mheshimiwa Mufti. Kwa viongozi watakaofaulu kwa kiwango cha juu, watatunukiwa vyeti vya ziada na motisha zinginezo zitakazopatikana.
MADARAJA YA KUTUNUKU
Kuna madaraja makuu manne ya kutunuku. Madaraja matatu (A, B+ na B) yanatuku kufaulu na daraja moja (C ) linatunuku kushindwa.
ALAMA | DARAJA | SIFA YA DARAJA | COMMENT |
100 -75 | A | AMAFAULU VIZURI SANA | EXCELLENT |
74- 64 | B+ | AMEFAULU VIZURI | BETTER |
64- 50 | B | AMEFAULU | GOOD |
49-0 | C | AMESHINDWA | FAIL |
-
MODULI NAMBA 1
- MODULI NAMBA 1:MUUNDO NA MIFUMO YA TAASISI
- MODULI NAMBA 2: RASILIMALI ZA TAASISI
- MODOULI NAMBA 3: MIRADI YA TAASISI
- MODULI NAMBA 4: TEHAMA
- KITABU MODULI YA PILI-RASILIMALI ZA TAASISI
- KITABU MODULI YA TATU-MIRADI YA TAASISI
- KITABU MODULI YA NNE-TEHAMA
- FOMU YA KUJIUNGA NA KOZI
- KITABU:MODULI YA KWANZA:MUUNDO NA MIFUMO YA TAASISI
0.00 average based on 0 ratings
Endelea na juhudi za kuitafuta picha ya msikiti wa kinondoni.
Naam vizuri sana
Hongera sana, mmefanya jambo zuri sana kwa kutengeneza mafunzo haya
Excellent, kazi kubwa sana na nzuri ya kujivunia.
Inapendeza kwa viongozi wa Bakwata katika ngazi zilizotajwa kupatamafunzo haya ili kusaidia kuwajengea uwezo wa kutekeleza majukumu ya kiuongozi katika maeneo yao.
Hii kweli ni Bakwata mpya, hongereni nyote mkiongozwa na Mufti
Ni jambo jema hongera kwa kuthubutu kulifanya hili mtandaoni, litakuza fikra za viongozi na utawala bora pia.
Hongereni sana baraza kwa kazi kubwa na nzuri
Jambo jema sana… Hongereni kwa kuanzisha hili, maoni yangu ni kwamba mafunzo haya yarudiwe tena na tena kwa sababu kuna wengine bado hawajapata wasaa kwa kipindi hiki kutokana na sababu mbali mbali. Allah awalipe zaidi tuzidi kuboresha program hii.