0 student

UTANGULIZI

Jina la KOZI  hii ni TEACHING METHODOLOGIES, lenye maana ya mbinu au njia za ufundishaji.

Mwalimu wa madrasa nchini Tanzania, anatumia ujuzi wake binafsi ama unaotokana na mafunzo maalumu au hana kabisa mafunzo na hivyo anajikuta ni mtu ambaye aitwa ni Mwalimu lakini hana mbinu za ualimu za kuweza kufanya kazi yake kuwa na ujuzi stahiki. Matokeo yake anaweza kutumia muda mrefu kufundisha sehemu ndogo sana ya somo na pengine asifikie malengo kwa sababu hana mbinu za kumfikisha huko.

Hali kadhalika Mwalimu huyo huyo anaweza kuwa pia hana mpangilio maalumu wa kufundisha na kujikuta hana mwendo unaotakiwa.

Moja kati ya fani zinazohitaji maarifa, ujuzi na stadi ni fani ya ufundishaji. Ufundishaji (ualimu) ni fani ambayo kila mjuzii wa kitu chochote lazima kuna chanzo na njia zilizo tumika kumfanya awe  mjuzi. Na kila mjuzi ana mjuzi wake. Hivyo katika kozi hii kila aliye mjuzi ni wajibu kwake kuwajuza wengine wasio na ujuzi kupitia njia zilizo bainishwa na huo ndio ufundishaji. Mwalimu wa madrasa nchini Tanzania anafundisha kwa njia ambazo anajua yeye mwenyewe huko alipo. Hatuna mfumo mmoja ambao unatuunganisha kwa pamoja kama nchi nzima. Kozi hii ni ya kwanza ambayo inaanza kutuunganisha nchi nzima kwa pamoja. Inshaa Allah naomba ilete mafanikio si ya kusoma na kufaulu mwalimu wa madarsa, bali ifungue na mambo mengine ya kuzipa madrasa zetu nguvu ya kutoa mafunzo kwa ufanisi mkubwa.

Mada zilizojadiliwa kwa upana ni mada kuu mbili zifuatazo:-

  • Maana ya ufundishaji
  • Mbinu za ufundishaji

MATARAJIO YA MAFUNZO

Mwisho wa mafunzo ya kozi hii, tunatarajia mwalimu wa madrasa aweze kujenga stadi katika maeneo yafuatayo;

  1. Kubaini maana ya mfundishaji na kumbaini mfundishwaji
  2. Kujenga mahusiano mazuri ya kimaadili kati yake na wanafunzi pia na wazazi
  • Kutambua kila njia ya kufundisha kwa faida zake na hasara zake.
  1. Kutambua nafasi yake kabla ya kuzifahamu mbinu mpya na mbinu alizokuwa akizitumia na hivyo kuboresha ufundishaji wake.
  2. Kuadaa mpango kazi wa ufundishaji
  3. Kuandaa somo vizuri la kufundisha katika kipindi husika
  • Kuandaa mthani na usahisahji wake
  • Kutathimini somo lake baada ya matokeo

HITIIMISHO

Kozi hii itajenga uwezo kwa walimu wa madrasa kuweza kuwa na utaratibu sawa kwa nia ya kuboeresha mafunzo ya madrasa nchi nzima ili kuweka viwango sawa vya ufundishaji.Kozi ya hii itumike kama ufunguo wa kujenga msingi imara wa madrasa zetu.

Instructor

BAKWATA ni Taasisi ya Waislam Tanzania inayounganisha taasisi zote za waislam Tanzania.

0.00 average based on 0 ratings

5 Star
0%
4 Star
0%
3 Star
0%
2 Star
0%
1 Star
0%
Sh20,000.00

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

wpChatIcon