1.Kwanza inabidi uwe unayo email binafsi, kisha uwe na internet(Kifurushi cha Data) kwenye simu au computer yoyote yenye internet
2. Ingia kwenye mtandao na Andika jina la chuo mtandao sehemu ya kuandika majina ya tovuti kama hivi: www.bakwataonlineacademy.ac.tz
3. Bonyeza Enter, kufungua chuo
4. Baada ya kufungua na kuona kilichopo, tafuta sehemu ya iliyoandikwa: Jisajili/Ingia na bonyeza , ukisha bonyeza utaona Login na chini yake utaona REGISTER kama ni mara ya kwanza kuingia, hii ni fomu ya kujisajili.
Kwenye REGISTER Utajaza user name(JINA) na Email yako na kisha jaza password yako utakayokuwa unatumia.
Kisha bonyeza : REGISTER
HATUA YA PILI
Tafuta sehemu iliyoandikwa hivi:
JAZA TAARIFA ZAKO KWA MAKINI, kisha jaza kwa kufuata maelekezo yaliyopo kwenye fomu kisha bonyeza ili utume taarifa zako kwa msajili.
Utapata maelekezo na utalipa karo kwenye Akaunti Maalum ya Mafunzo chini ya Ofisi ya Mufti na kuanza mafunzo kwenye akaunti yako ya masomo moja kwa moja kwa kutumia simu au kompyuta.
Utaingia muda wote darasa mtandao kusoma kozi yako kwa kutumia:
User name yako na Password yako
Hizo ulizosajili user name na password ni kama funguo za darasa lako, zitunze vizuri na kwa usalama.