2 students

URASIMISHAJI ELIMU YA MASHEIKH

KATIKA KOZI HII UTASOMA MODULE 4 ZIFUATAZO

MODULI NAMBA 1: MUUNDO NA MIFUMO YA TAASISI

MODULI NAMBA 2: RASILIMALI ZA TAASISI

MODOULI NAMBA 3: MIRADI YA TAASISI

MODOULI NAMBA 4: TEHAMA(TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO

MUONGOZO KUHUSU ELIMU KWA NJIA YA MASAFA

WALENGWA WA KOZI HII NI:

Ni Masheikh na viongozi wote kuanzia Mkoa, Wilaya, Kata, Misikiti,  JUVIKIBA, Umoja wa Wakina mama Bakwata , walimu wa madarasa, maimamu na wale wote watakaohitaji maarifa kuhusu uongozi, utawala bora na Tehama na kupata cheti rasmi kinachotambuliwa na taasisi za kiislam Tanzania kilichosaininiwa na MUFTI wa Tanzania.

USOMAJI, UPIMAJI ,KUTUNUKU NA MADARAJA YA KUTUNUKU

USOMAJI

Kiongozi atasoma moduli hizi tatu kwa njia ya masafa (mtandaoni) kupitia tovuti ya chuo cha BAKWATA MTANDAONI kwa kupakua (download) kitabu cha moduli kisha atasoma moduli moja moja na kujibu maswali ya moduli husika. Pia, kupitia video ambazo zitawekwa kwenye tovuti.

UPIMAJI

Kiongozi baada ya kusoma moduli, atapimwa ufahamu wake kwa kujibu maswali baada ya moduli. Kila moduli itapimwa kwa uzito wa alama 100, hivyo ufaulu wa kiongozi utapimwa kupata alama 50 kuwa amefaulu moduli husika. Alama chini ya 50 maanake moduli hiyo hajafaulu.  Kiongozi akimaliza kujibu maswali atatakiwa kuyatuma kwa njia ya mtandao (email) ili yapate kusahihishwa.

KUTUNUKU

Baada ya  kukamilisha mafunzo ya uongozi na utawala bora, kiongozi atakayefaulu moduli zote tatu atatunukiwa cheti cha kufaulu kwake. Wastani wa ufaulu kwa moduli zote tatu ni alama 50. Maanake kama mduli zote tatu zikijumlishwa kwa pamoja kasha kugawanywa kwa tatu, wastani ukifikia 50 kiongozi atakuwa amefaulu na kuwa na sifa ya kutunukiwa.

Mfano kama moduli ya kwanza amefaulu kwa alama 70, moduli ya pili kwa alama 60 , moduli ya tatu  kwa alama 80 na moduli ya 4 kwa alama 75,  hivyo wastani wa jumla wa kutunukiwa ni 70 ( maanake 70 + 80 + 60 + 75= 285. Hizo alama 285 gawia kwa 4 ni sawa na alama 71.25). Hii ni kuweza kumjengea ufaulu kiongozi kwa sababu kuna moduli ambazo anaweza kuwa amezifahamu zikambeba kufaulu kwa zile moduli ambazo atakuwa hajazifaulu vyema.

Cheti kitatolewa na kusainiwa na Mheshimiwa Mufti. Kwa viongozi watakaofaulu kwa kiwango cha juu, watatunukiwa vyeti vya ziada na motisha zinginezo zitakazopatikana.

MADARAJA YA KUTUNUKU

Kuna madaraja makuu manne ya kutunuku. Madaraja matatu (A, B+ na B) yanatuku kufaulu na daraja moja  (C )  linatunuku kushindwa.

ALAMA DARAJA SIFA YA DARAJA COMMENT
100 -75 A AMAFAULU VIZURI SANA EXCELLENT
74- 64 B+ AMEFAULU VIZURI BETTER
64- 50 B AMEFAULU GOOD
49-0 C AMESHINDWA FAIL

 

Instructor

BAKWATA ni Taasisi ya Waislam Tanzania inayounganisha taasisi zote za waislam Tanzania.

0.00 average based on 0 ratings

5 Star
0%
4 Star
0%
3 Star
0%
2 Star
0%
1 Star
0%
Sh50,000.00

One thought on “UONGOZI,UTAWALA BORA NA TEHAMA

  1. Inapendeza kwa viongozi wa Bakwata katika ngazi zilizotajwa kupatamafunzo haya ili kusaidia kuwajengea uwezo wa kutekeleza majukumu ya kiuongozi katika maeneo yao.

  2. Ni jambo jema hongera kwa kuthubutu kulifanya hili mtandaoni, litakuza fikra za viongozi na utawala bora pia.

  3. Jambo jema sana… Hongereni kwa kuanzisha hili, maoni yangu ni kwamba mafunzo haya yarudiwe tena na tena kwa sababu kuna wengine bado hawajapata wasaa kwa kipindi hiki kutokana na sababu mbali mbali. Allah awalipe zaidi tuzidi kuboresha program hii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

wpChatIcon